MunaLove "Bila Mwanangu Nisingeokoka Sikuwa Najua Biblia"

Baada ya mfanyabiashara, Muna Love, kuokoka na kuachana na maisha yale ya kidunia aliyokuwa akiishi, amezungumza na Global TV na kufungukia maisha yake ya sasa ndani ya Yesu. Muna amesema kwamba mitihani aliyoipata wakati wa kumuuguza mwanae Patric aliyezaa na mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson, ndiyo hasa iliyomfanya arudi kwenye mikono ya Mungu, na pengine kama mwanae asingeumwa labda asingeokoka.

Kuhusu sakata lililowahi kuvuma la Muna kuiba nguo ya ndani ya Muigizaji Wema Sepetu ambaye alikuwa shoga ake pete na kiidole, Muna amesema malkia huyo wa Bongo Muvi, alikuwa havai nguo za ndani ila mashabiki wame panic bure na hawakumuelewa dhamira yake. Kuhusu mzazi mwenziye Casto Dickson, Muna amekataa kuzungumzia.

VIDEO:

Top Post Ad

Below Post Ad