Muuguzi Awachoma Sindano za Sumu Wagonjwa 20 Wenye Hali Mbaya ili Wafe

Muuguzi Awachoma Sindano za Sumu Wagonjwa 20 Wenye Hali Mbaya ili Wafe
Muuguzi aitwae Ayumi Kuboki mwenye miaka 31 anatuhumiwa kuwachoma sindano za sumu Wagonjwa 20 wenye hali mbaya ili wafe kwenye zamu ya Muuguzi mwingine.

Ayumi alipokuwa akihojiwa na Polisi alisema kuwa alifanya hivyo ili kuepukana na shida ya kuwaelezea familia za wafiwa chanzo cha vifo vya ndugu zao.

Kwa mujibu wa sheria za Hospitali ya Oguchi ya mjini Tokyo ambayo Ayumi ndipo anapofanyia kazi zinasema kuwa Muuguzi ndie mwenye wajibu wa kuwapa taarifa ndugu endapo Mgonjwa atafariki kwenye zamu yake na ndio maana alifanya hivyo kukwepa kadhia hiyo.

Aidha uchunguzi wa Polisi unasema kuwa Ayumi aliwapa sumu hata Wagonjwa wengine ambao hawakuwa na hali mbaya. Kwa sasa Ayumi anashikiliwa na jeshi la Polisi la nchini humo kwa ajili ya kupandishwa kizimbani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad