Mwanamitindo Ang'atwa na Papa Akipiga Picha Baharini

Mwanamitindo Ang'atwa na Papa Akipiga Picha Baharini
Kisiwa cha Exuma nchini Bahamas kina umaarufu wa michanga meupe iliopo ufuoni mwa bahari , maji masafi na maneo mengi ya kuvutia.

Hivyobasi mwanamitindo Katarina Zarutskie alipozuru ufuo huo pamoja na mpenzi wake, mwezi uliopita alikuwa na ari ya kutumia maeneo mazuri ya fukwe hiyo ya bahari.

Baada ya chakula cha mchana na familia katika eneo linalojulikana kama Staniel Cay, Katarina aliwaona watu waliokuwa wakiogelea karibu na papa mchanga katika eneo moja.

Licha ya familia ya mpenzi wake kuwa na wasiwasi, alikuwa yuko tayari kuingia katika maji hayo ili kupiga picha nao.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuanza mafunzi ya shahada mbili za uuguzi na biashara mjini Miami na sio mgeni wa maswala ya bahari baada ya kukuwa akifanya michezo ya baharini nyumbani kwao huko mjini California.

''Kutokana na ufahamu wangu wa kuteleza majini na kuogelea chini ya maji najua kwamba papa wachanga huwa salama'', aliambia BBC .

Nimeona watu wengi wakipiga picha nao katika mtandao wa Instagram

Samaki huyo amekuwa kivutio cha watalii, akizurura katika gati mbali mbali na kuonekana katika maelfu ya picha zilizosambazwa katika mitandao.

Anasema kwamba baada ya dakika chache za kuchukua mkao , raia mmoja wa eneo hilo alimshawishi kuolea majini huku mwili wake ukiangalia juu.

''Wakati huo watu walikuwa wameanza kupiga picha , nilipokuwa nikilala kuangalia juu nilihisi kitu kimenivuta chini'', alisema.

Babake mpenzi wake alikuwa akimpiga picha Katarina wakati huo, na kwa bahati nzuri akapata kisa chote katika kamera yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad