MAREKANI : Mwanamitindo Mashuhuri wa Marekani, Farren Jean Andrea anayejulikana zaidi kama Fucci ametangaza kuwa ni muathirika wa Virusi vya Ukimwi 'VVU.'
_
Fucci aliyepata umaarufu kwa kufanya kazi na Mwimbaji Rihanna, Bella Hadid, Jhene Aiko na miongoni mwa wengine wengi alitangaza uathirika wake kupitia ukurasa wake wa Twitter, Jumatano ya tarehe 25 Julai.
Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 25 aliweka ujumbe wenye taarifa hiyo ambapo alibainisha ilivyo kuwa ngumu kwake kuweka wazi hali hiyo ya VVU na kuomba watu wamuombee.