Mwanamke mmoja nchini Saudi Arabia amekamatwa baada ya kukimbilia juu ya steji na kumkumbatia mwanamuziki wa kiume wakati wa tamasha.Ripoti zimeeleza.
Majid al-Mohandis alikuwa akitumbuiza kwenye tamasha mjini Taif magharibi mwa nchi hiyo, wakati mwanamke huyo alipopanda kwenye steji.
Video zilizowekwa mtandaoni ziimuonesha akiwa kamkumbatia mwanamuziki huyo huku maafisa wa usalama wakijaribu kumvuta mwanamke huyo.
Wanawake nchini Saudi Arabia hawaruhusiwi kujichanganya na wanaume wasio na undugu au mahusiano nao wakiwa hadharani.
Mohandis ambaye tovuti yake inasema ''yeye ni mwana mfalme katika uimbaji wa kiarabu'',hajasema lolote kuhusu tukio hilo.Muimbaji huyo mzaliwa wa Iraq ,ambaye pia ana uraia wa Saudia, aliendelea kutumbuiza baada ya tukio.
Mwendesha mashtaka atazingatia sheria ya udhalilishaji dhidi ya mwanamke huyo, Polisi ililiambia gazeti la Okaz na shirika la habari Efe.
Nchi hiyo ina sheria kali kuhusu kupiga marufuku unywaji pombe, mavazi ya kimagharibi na masuala ya jinsia.
Mazuio ambayo yaliwekwa dhidi ya wanawake kushiriki matukio ya Umma nchini humo yalianza kulegezwa mwaka uliopita chini ya mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na mwana mfalme Mohammed bin Salman.
Wanawake waliruhusiwa kuhudhuria matamasha na michuano ya mpira wa miguu kwa mara ya kwanza, kisha nchi hiyo ilihodhi tamasha la kwanza lilifanywa na mwimbaji wa kike, kutoka Lebanon Hiba Tawaji, mwezi Desemba.
Wanawake waliruhusiwa kuendesha magari tangu mwezi Juni.
Lakini bado kuna mazuio muhimu yameendelea kuwepo kama vile mavazi.Wanawake walioonekana wakimkumbatia mwanamuziki huyo walivaa Niqab, vazi linalovaliwa kichwani likionyesha macho pekee.
Mwanamke Akamatwa kwa Kosa la Kumkumbatia Mwanamuziki wa Kiume Stejini
0
July 16, 2018
Tags