Mwanamuziki Childish Gambino Aliyeimba This is America Kufikishwa Mahakamani


Mcheza filamu na mwanamuziki ‘Donald Glover; a.k.a ‘Childish Gambino’ anaetamba na wimbo wake “This is America” anatarajiwa kupelekwa mahakamani na Lebo yake ya zamani baada ya kutolipa mapato aliyoyapata katika streams za albamu zake akiwa chini ya lebo hiyo.

Taarifa kutoka katika chombo kimoja cha habari cha nchini Marekani kimesema kuwa lebo ya ‘Glassnote Entertainment Group’ wamefungua kesi ya madai ya fidia dhidi ya ‘Childish Gambino’ kwa madai kuwa amepata kiasi cha dola za Marekani laki saba ($700,000) katika stream (watu kuangalia kazi zake mitandaoni) na wala hawajalipwa hata thumni ya mapato hayo ambayo ni sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 1.5 za kitanzania.

Chilidish Gambino aliachia albamu zifuatazo akiwa chini ya lebo ya ‘Glasssnote’ ‘CAMP 2011’, ‘BECAUSE THE INTERNET 2013’, ‘AWAKEN,MY LOVE 2016’

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad