Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James ameouomba radhi umma wa Watanzania kufuatia kauli yake iliyochukuliwa kama udhalilishaji kwa walipa kodi
Kheri alisema kuwa ‘CCM ndiyo inayoamua maendeleo yaje au yasije na hakuna mwananchi anayeweza kuchukua hatua yoyote dhidi ya chama hicho'
Kwa kauli yake amesema kuwa 'nachukua nafasi hii kuwaomba Radhi Watanzania Wenzangu wote walio kerwa na ujumbe huo'
Ameongeza kuwa anawashukuru viongozi wote wa kisiasa na kiraia walio nikosoa na kunikemea kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ninawashukuru sana'