Naamini Liverpool Watakuwa Mabingwa Msimu huu – Mourinho

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amefunguka na kusema kuwa anaamini Usajili ambao wameufanya klabu ya Liverpool wananafasi kubwa zaidi ya kuchukua taji la ligi kuu nchini Uingereza.

Mourinho ameyaongea hayo kwenye press yao baada ya mchezo wao wa kirafiki waliocheza jana dhidi ya Ac Milan huko nchini Marekani na kufanikiwa kushinda goli 9-8 katika kipengele cha mikwaju ya penalti kwani muda wa kawaida wa dakika 90 waliweza kutoka sare ya goli 1-1.

Lakini pia Liverpool wao wa;licheza na wapinzani wakubwa wa Manchester United na Liverpool kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 magoli ya Mohamed Salah pamoja na Goli la Sadio Mane huku Man City wakipata goli lao kupitia kwa winga wao Leroy Sane.

Mourinho amemsifia Klopp na kusema“Nadhani kama una pesa, ikiwa unawekeza vizuri, ni bora kuliko kuwa na benki. Kwa sababu viwango vya riba ni ndogo sana, “Mourinho aliongeza.



“Tatizo ni lazima uwekeze vizuri na kwa uaminifu nadhani walifanya vizuri sana, kwa sababu kila mchezaji waliomnunulia ni wachezaji bora. Ninafurahi kwa hilo”

Hayo yanakuja baada ya Majogoo Liverpool kufanya usajili mzuri sana unaokadiriwa kufikia Euro mil 170 baada ya kumsajili mlinda mlango Alisson Becker kutoka AS Roma.

Liverpool wamefanya usajili wa wachezaji wanne wazuri ambao ni Naby Keita kutoka RB Leipzing,Shakiri kutoka Stoke City,Fabinho kutoka Monaco,Alisson Becker kutoka AS Roma ambapo gharama yao inakadiriwa kufikia Euro mil 170.



By Ally Juma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad