'Nabii' Aliyeshindwa Kumfufua Mfu Akamatwa na Polisi

Maafisa wa polisi nchini Ethiopia wamemkamata kijana mmoja anayejiita 'nabii' kwa jina Getayawkal Ayele baada ya kushindwa kumfufua mfu aliyefariki siku nne zilizopita.

Tukio hilo lilifanyika katika mji wa Galilee huko Wollega magharibi mwa Ethiopia.

Kanda ya video ya 'nabii' huyo ikiita jina la mfu huyo kwa lengo la kumfufua ilisambazwa sana katika mtandao wa facebook.

Kanda hiyo ya video inaonyesha 'nabii' huyo akilala kando ya mwili huo na kuita jina la marehemu.


Awali alikuwa amekwenda kwa familia ya mfu huyo kwa jina Belay Bifu na kuwahubiria kuhusu habari ya Lazurus, vile Yesu alivyomfufua, muhubiri kutoka mji wa Dhinsa Dabela aliambia BBC.

''Niliona watu wengi wakikimbia kuelekea kule kaburi hilo lilikokuwa wakisema Belay anakaribia kufufuka. Niliwashauri watu kutomuamini nabii huyo lakini walinifukuza wakisema sina imani'', muhubiri huyo alisema.

Nabii huyo baadaye aliwafanya watu kuchimba kaburi , na kuchukua kipande cha nguo kilichotumika kumfunga marehemu na kuanza kumwambia Belay amka tena na tena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad