Naibu Waziri Agomea Uzinduzi Wa Majengo Ya Chuo Cha Afya Cha Waganga Wasaidizi Mkoani Mara

Naibu Waziri Agomea Uzinduzi Wa Majengo Ya Chuo Cha Afya Cha Waganga Wasaidizi Mkoani Mara
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amegoma kuzindua Majengo ya chuo chá Áfya chá Waganga Wasaidizi Mkoani Mara kutokana na kutoridhishwa na Matumizi ya fedha ya kiasi cha shilingi Milion 500 kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Majengo katika Chuo hicho.

Hayo yamejiri mapema jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua shughuli za ujenzi na ukarabati wa Majengo ya chuo hicho kilichopo Musoma, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika kukagua hali ya utoaji huduma za afya Mkoani hapo.

“Nimekuja hapa, kazi ya milioni 500 sijaiona kabisa ,kilichofanyika mmepiga rangi, kuta mbovu na Siwezi kuwa katika dhambi ya kuhararisha, kwahiyo nimegoma uzinduzi wa Majengo haya, na nimeagiza kwa chuo kupata maelezo kwa wote walishiriki na kuahidi kuwachulia hatua wote walishiriki ” alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile alitoa onyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Juu ya fedha nyingine zilizopelekwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo Saba vya utoaji wa huduma za Afya katika mkoa wa Mara na kumtaka kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha z vituo hivo ili viweze kuwasaidia wananchi wa Mara.

“Tumeleta tena fedha zingine kwaajili ya ujenzi wa vituo vya Áfya saba, naomba hizo fedha za umma tukazisimamie vizuri kwa ukamilifu, kama ukaona wenzako hawaendi katika njia sahihi, toa taarifa ili ujiokoe wewe, na wewe ukiwa katika sehemu ya kuhararisha ile dhambi dhoruba hii na wewe itakukumba ” alisema Dkt.Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile alitembelea kituo chá Áfya chá Bunda ambacho kinatambulika kama Hospitali ya Wilaya Dkt. Ndugulile aliagiza kusimamishwa kazi kwa Mganga Mkuu wa Mji wa Tarime kutokana na uzembe wa usimamizi mbovu wa huduma za afya katika kituo hicho, huku akimtaka Mkuu wa Wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili kuhakikisha anasimamia agizo hilo.

“Mambo haya yote yanatokea kwasababu ya usimamizi mbovu Kwaiyo nimeagiza Mganga Mkuu wa Mji (TMO) asionekane hapa, kamati ya mkoa wamchukue aletwe mtu mwingine anaeweza kusimamia, huyu mtu hatufai akapangiwe majukumu mengine, na Mkimruhusu tutaanza kuwajibishana sisi, tunataka kuijenga Bunda mpya ” alisema Dkt. Ndugulile.

Vilevile Dkt. Ndugulile alimwagiza Mganga mkuu wa mkoa wa kupitia upya Matumizi matumizi ya jengo jipya lililojengwa kwaajili ya kuhifadhi maiti Kwani haliendani na mahitaji kutokana na ukubwa wake, hivyo kuagiza kubadilisha matumizi ya jengo hilo na kulifanya kuwa jengo la x-ray.

“nimetembelea jengo la mochwali, jengo ni kubwa kuliko hata jengo la mochwali lá Muhimbili, sambamba na hilo nimeambiwa Kwamba kuna vifaa vya x-ray vimeletwa, Sasa nimetoa maelekezo Kwamba tubadilishe matumizi, lile jengo tunaweza kutumia kwa huduma za jengo la x-ray, nitaagiza wataalamu wangu waje kupitia jengo hilo ili tufunge vifaa vya x-ray, kazi ianze ” alisema Dkt Ndugulile.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad