Naibu Waziri wa Afya Kusamsaka 'Mchawi' wa Vifo vya Kina Mama Wajawazito

 Naibu Waziri wa Afya Kusamsaka 'Mchawi' wa Vifo vya Kina Mama Wajawazito
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kutafuta chanzo cha ongezeko la vifo vya kina mama wajawazito licha ya asilimia 80 ya kinamama kujifungulia katika vituo vya afya.


Dkt. Ndungulile ametoa agizo hilo Mkoani Simuyu katika ziara yake ya Kikazi Kanda ya ziwa baada ya kupewa taarifa ya hali ya afya ilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini.

Katibu Tawala huyo amesema kuwa Idadi ya vifo hivyo imeongezeka hadi kufikia vifo 48 vya kina mama wajawazito huku sababu kuu ya vifo hivyo ikiwa ni kutokwa na damu nyingi, Kifafa cha Mimba na upungufu wa damu.

Dkt. Ndungulile, ametoa maagizo ya kutafuta chanzo cha tatizo hilo huku akiomba viongozi wa Mkoa wa Simiyu kutafuta watu wanaoshi na virusi vya Ukimwi waliokatisha dawa za kufubaza makali ya Ukimwi lakini pia akitoa onyo kwa wazazi kulipishwa dawa pamoja na maji.

Mwezi Mei mwaka huu katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) Ofisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Uuguzi na Ukunga, Moris Hiza alisema chanzo cha vifo vya wajawazito kufariki inatokana na wingi wa wagonjwa huku wahudumu wakiwa wachache.

Hiza alisema kwamba  "kwa Tanzania takribani mkunga mmoja anahudumia wajawazito kuanzia 20 hadi 25 kwa siku huku kwa mujibu wa takwimu za kimataifa ilitakiwa mkunga mmoja amhudumie ipasavyo mjamzito mmoja kuanzia ngazi za awali hadi wakati wa kujifungua na hata kumhudumia mtoto".

Naye Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (Tama), Feddy Mwanga, Mwezi mei mwaka huu katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), aliweka wazi kwamba hali ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini kwa kila vizazi hai 100,000 vifo vya watoto  wachanga ni 556


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad