Nampenda Sana Huyu Kaka Mpaka Naona Najipendekeza

Habari wadau, mimi ni msichana mwenye umri wa 26yrs.

Nina mpnzi wangu ambaye nampenda sana, kiasi kwamba tukitofautiana kauli huwa inanipa shida sana,najihisi hadi kuumwa, ila kwake yeye huwa naona kama anachukulia poa.

Jana usiku tumepishana kauli nimeumia sana na mpaka sasa hatujawasiliana, kila mmoja ameuchuna, pia kinachonikwaza ni kwamba kila tukigombana mimi ndio huwa lazima niombe msamaha,hata kama kakosa yeye, ila leo nataka niendelee kuuchuna,for this, am I correct or not.

Pia nipeni mbinu za kumpenda mtu kiasi kwa sababu nimegundua too much is harmful.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad