Nape Nauye Aomboleza Kifo cha Maji Marefu

Nape Nauye Aomboleza Kifo cha Maji Marefu
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu atakumbukwa kwa busara na ucheshi wake.

Nape aliyasema hayo leo Julai 4, 2018 baada ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Prof Majimarefu alifariki dunia Julai 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Nape amesema Majimarefu alikuwa rafiki wa kila mtu. "Alikuwa anapenda kusema ukweli bila woga, ni mpenda watu na mwenye ushirikiano.”

Mbali na hayo Nape amesema marehemu Majimarefu alikuwa na mchango mkubwa hasa katika michezo.









Tags

Top Post Ad

Below Post Ad