Natamani Kucheza na Wema Sepetu – Aslay


Muimbaji Aslay amedai anavutiwa na muigizaji wa mrembo Wema Sepetu katika filamu na kudai endapo siku ataamua kuingia katika uwanja wa uigizaji rasmi basi ni lazima atafanya naye kazi.


Akiongea kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Aslay amedai Wema Sepetu ni mtu wa kwanza ambaye anatamani kufanya naye kazi.

“Endapo ntaigiza basi msanii wa kwanza kufanya naye kazi ni Gabo Zigamba kwa sababu ananivutia sana na kazi zake ila kwa upande wa kike natamani kucheza na Wema Sepetu, Irene Uwoya, Riyama na wengine wengi”, amesema Aslay.

Pamoja na hayo, Aslay ameendelea kwa kusema “sijawahi kufikiria kama ninaweza kuigiza ila huwa najaribu tu kidogo kidogo kuigiza tatizo kukaa mbele ya kamera ndio shida. Kiukweli navutiwa na movie ila kama mashabiki zangu wananiona najua kuigiza basi nashukuru sana na nitajaribu kufanya hivyo siku moja”.

Mbali na hilo, Aslay amesema katika vitu ambavyo huwa vinamchukiza zaidi ni kuona baadhi ya watu wakimzushia sifa mbaya kuwa anaringa jambo ambalo sio la kweli kwa upande wake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad