Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ameiagiza Tume ya vyuo vikuu nchini TCU kuongeza kasi ya kuhakiki ubora wa vyuo vya elimu ya juu na vitakavyobainika kukosa vigezo hata kiwe cha serikali kifungiwe kwani suala la ubora wa elimu ni jambo la lazima kwani hakuna haja ya kuwa na msururu wa vyuo visivyokuwa na tija.
Prof Ndalichako ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonyesho ya vyuo vikuu ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
Wakati akizindua maonyesho hayo Prof Ndalichako amevitaka Vyuo vikuu kutafuta suluhu changamoto zinazoikumba jamii na kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo,viwanda ambapo baadhia ya vyuo vimemweza kuhusu tafiti walizofanya katika maeneo hayo.
Katika maonyesho hayo baadhi wanafunzi wamejitokeza kupata taarifa za namna ya kujiunga na vyuo vya ndani na nje ya nchi na kupatiwa maelezo ya kina.