NEC Yatangaza Uchaguzi Mdogo Jimbo la Buyungu

NEC Yatangaza Uchaguzi Mdogo Jimbo la Buyungu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itafanya uchaguzi mdogo kwenye Jimbo la Buyungu, Mkoani Kigoma na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara.



Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema uchaguzi huo utafanyika tarehe 12 mwenzi ujao (Agosti) na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 8 hadi 14 mwenzi huu (Julai).

“Uteuzi wa Wagombea utafanyi katarehe 14 Julai, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 15 Julai, hadi tarehe 11 Agosti, mwaka huu na siku yauchaguzi itakuwa ni tarehe 12 Agosti mwaka huu,” alisema.

Jaji Kaijage amebainisha kwamba Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo hilo la Buyungu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Ndugu Job Ndugai.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Buyungu katika Halmashauri ya Kakonko Mkoani Kigoma kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Kasuku Samson Bilago,” alisema Kaijage.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad