Ngono Sehemu ya Kazi: Je, ni Kweli Huambatana na Mikosi?
0
July 26, 2018
Miaka ya nyuma kidogo kuna rafiki yangu aliwahi kufanya ngono na dada mmoja ofisini wakiwa peke yao overtime. Jamaa alinisimulia kila kitu sababu alikuwa ni mshikaji wangu sana. Miezi michache baadaye kazi ikaharibika na jamaa akafukuzwa kazi.
Siku moja nikawa napiga stori na wenzangu na tukawa tunaongelea swala la watu kufanya ngono maofisini. Nikawaambia kuwa ukifanya zinaa ofisini na mfanyakazi mwenzako basi huwa kuna mikosi itakupata na utafukuzwa kazi hata kama hakuna mtu atakayejua kuwa umefanya ngono ofisini.
Jamaa mmoja akakiri mbele yetu na kusema kuwa ni kweli hata yeye aliwahi kufanya sex akiwa ofisini na miezi sita baadaye alifukuzwa kazi katika mazingira ya kutatanisha sana. Akatuambia kwamba baada ya tendo lile mikosi ikaanza kumwandama na mwisho wa siku akafukuzwa kazi kwa makosa ambayo hakutegemea kama angeyafanya.
Kuna mifano mingi sana isiyo rasmi ambayo inaelezea namna ngono au zinaa inavyoweza kuleta mkosi katika kazi yako kama ikifanywa ofosini mahali ambapo unapata riziki yako ya kila siku. Kuna watu wanasema kwamba ukifanya zinaa ofisini unakuwa umekinajisi kibarua chako.
Je! Kuna ukweli katika hili? Kama siyo kweli ni kwanini wanaofanya ngono ofisini wengi wao huishia kufukuzwa kazi hata kama tendo la zinaa walilofanya huwa ni siri yao na halijulikani mbele za watu?
Tags