NHIF Haitowalipia Gharama Wanaotoa Mimba

Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF umefafanua kuwa hautahusika  kuwalipia gharama za matababu watu walioumia katika majanga ya uvunjifu wa sheria kama utoaji mimba wa makusudi na ujambazi.

Ufafafanuzi huo umetolewa na Kaimu Meneja wa Mfuko wa  Bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Ruvuma Doto Miraji wakati akizungumza na waratibu wa NHIF na CHF wa halmashauri za mkoa wa Ruvuma na wanaoshughulikia huduma hizo katika hospitali za misheni mkoani humo.

Kwa upande wao Waratibu wa NHIF na CHF mkoani Ruvuma wanasema kuwa wamejipanga kusimamia vizuri mpango wa matibabu ya bima ya afya kuelekea azma ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi anatibiwa kupitia bima ya afya na kuondokana na matatizo ya wananchi kupoteza maisha kwa kukosa fedha za matibabu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad