Ni Afadhali Rais Magufuli Tunaziona Hata Ndege, Flyovers, Ukuta wa Mererani na Mengine, Huko Nyuma Je?

Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Km ndege zitatuletea watalii wengi, basi pesa ya kuboresha huduma za afya itakuwepo, na usimamizi bora wa matumizi ya pesa hiyo wala sina shaka, hapa kazi tu. Hao watalii wakija hawatapata tabu sana kuhusu usafiri wa ndani, kwani ndege ipo, flyover ya kupunguza foleni ipo, na wafanye kazi siku hizi wanatoa huduma bora bila kudai rushwa. Hakika watalii watafurahi sana, kisha wataenda simulia kwao, na hapo ndipo tutakapoanza kupata watalii wengi zaidi mpaka mshindwe pa kuwaweka. Wengi wenu mtaanza kupangisha nyumba zenu kwa watalii na kuwabagua wazawa, kisa wanawalipa dola. Biashara za migahawa na hotel zitaongezeka, kisa zinalipa sana. Wasusi wa nywele maisha yatabadilika, maana watalii hupenda kurudi kwao wakiwa wamesukwa kiafrica. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. Huniambii kitu Kwa Magu!! Huyu ni Jemedali haswaaaaa!!!
    Historia anyoiandika kiukweli hata Mwalimu… Itabidi tujadili.
    Mlume katufanyia vitu Haswa kwa Miaka Miwili na Nusu hakuna Mfano wala comparizone!!
    Huyu ni Game changer... Mlisema hawezi … Kafanya Kweli na anaendelea Kufanya…. Mtapata Tabu sana…. Mtamwelewa muda si Mrefu….. Hapa Kazi Tu.

    Magu… TINGA TINGA… Mkulu Mlungu akutaze Ngweeeee!!!!
    Uli mdodo wa Kukayaaaaaa……!!!
    Milimo ili Baho Mwaha….!!! Magufuli Oyeeeeeeeeeeeee!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad