Naombeni Ushauri, Mimi ni Mbongo Mtanzania halisi Msichana wa miaka 32 , Mimi nina tatizo la kutopenda wanaume wenye ngozi nyeusi hasa Wabongo ndo kabisa na walivyowaswahili, Basi nimekuwa nikidate na wanaume Wazungu tu mpaka sasa ila wengi wao wanakuwa available ni vibabu so ndoa hakuna unakuta wana wake zao huko kwao, Umri unaenda na ninataka niolewe ila sipendi weusi , Nasikia hadi kinyaa nikidate nao, Nifanyaje hii hali initoke?
Jasmini
Wewe mwenyewe cheusi, babako mweusi na mama pia mweusi !!! Halafu wewe unajifanya wa ulaya ulaya?
ReplyDeleteNa nakuhakikishia ukifikisha tu 35 waoaji hutawaona na wala hao wazungu utawasikia tu
akifikisha miaka 35 mbona ni umri mdogo tu labda huko bongo ndiyo umri mkubwa watu wanaolewa kwa umri wowote vile umri si hoja ni watu wakipendana tu na Ulaya watu hawaolewi mapema wala hawazai mapema
ReplyDelete