Nisha apost video mtandaoni inayomuonyesha Akibadilishana Ulimi na Mzungu

Msanii wa filamu Salma Jabu aka Nisha amewaacha mdomo wazi mashabiki wake wa filamu baada ya kupost video mtandaoni ambayo inamuonyesha akiliwa denda na mpenzi wake mpya mzungu.

Muigizaji huyo amedai hawezi kukaa kimya bila kumuonyesha mpenzi wake huyo licha ya mashabiki wengi mtandaoni kumdhihaki.

“Ni ngumu sana kuficha hisia zangu kwa mtu nnayempenda, nimeshakuwa na m-black, Mwarabu ila kote niliambulia usaliti na uongo wa mapenzi, niliwahi sikia Wazungu wana mapenzi ya kweli kuliko Waafrica, kujaribu si mbaya.

“Me ni msafiri sijafika bado, na Mwenyezi Mungu anajua kama hapa ndo mwisho wa safari yangu au inaendelea, kikubwa nimeshampata na maneno sijali,’ amesema Nisha.

Katika post nyingine Nisha amesema;“Walimwengu sijui mna nini, nikiibiwa bwana mnanyamaza kimya, nikiwa na wa rika langu ben 10, akinizidi umri kizee, au mlikuwa mnafurahia kujiita bachelor? Sasa nimeshampata bado maneno kedekede. Yeye na mimi kwani tuna kasoro gani? Au mimi nimezaliwa niliye tu na kuibiwa?”

A post shared by Salma Jabu Nisha (@nishabebee) on
.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani sijui lini huu ushamba utatuisha lini , wanawake wa kibongo wengine ni wapumbavu, yaani Nisha unatuwekea nini hiyo. kama mzungu si angekutafuta akiwa kijana?yaani tunashoboka. alafu nyie mastaa mnatufanya wanawake wa bongo kusomeka kama malaya kimataifa. una jizee lako si utuliye nalo ndani?unahu:!!!!hadi mitandaoni. yaani mnanikera. watu tunaangalia maisha ya kesho.nyie si ndio wazee wa kesho mtakaosumbua serkali kwamba, ooh serkali haiwadumii wazee mtataka misaada uzeeeni na kuwasumbua watoto wenu. andaa maisha ya kesho acha kushoboka kwa mambo yaso yamsingi. natamani sana nikusikie Nisha, una biashara kubwa, nikuone unakuja na uvumbuzi mpaya.tuonyeshe maendeleo sio mabwana wa siku mbili wametoweka.mtoto wako baadae ataitwa mtoto wa nani kama wewe mwenyewe huna maadhili? jiulize kesho yako nini.acha shobo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad