Obi amethibitisha kuwa alipata taarifa za kutekwa kwa baba yake lakini watekaji walimpa onyo asimwambie mtu yoyote au mamlaka za usalama nchini Nigeria, kwani angefanya hivyo baba yake angeuwawa.
“Waliniambia kwamba wangemuua baba yangu kama ningetoa taarifa kuwa ametekwa kwa mtu yoyote au mamlaka za usalama” Obi Mikel
Watekaji lengo lao kubwa lilikuwa ni kujipatia pesa kutoka kwa staa huyo kwani walimuagiza atoe dola za kimarekani 28000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 60 za kitanzania ili wamuachie baba yake akiwa hai bila kumdhulu kwa chochote.
Baba yake Obi na dereva walikuwa safarini kutoka Jos kuelekea sehemu za kusini mwa Nigeria kwa ajili ya mazishi lakini walitekwa na baadae kufanikiwa kuokolewa na Polisi July 2 ikiwa imepita wiki moja toka taarifa za kutekwa kwao ziliripotiwe kwa familia.