Okwi na Bocco Waiingizia Simba Milioni 300

Okwi na Bocco Waiingizia Simba Milioni 300
INAELEZWA kuwa, kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mashabiki wengi ndio waliingia uwan¬jani na kushuhudia mechi za Simba ambayo ilikuwa na wachezaji wenye mvuto wa juu, Emmanuel Okwi na John Bocco.

Simba ndiyo timu iliyoweka reko¬di msimu uliopita kwa kutazamwa na mashabiki wengi zaidi kuliko timu nyingine zote hali iliyoifanya kupata mapato mengi zaidi.
Okwi na Bocco kwa pamoja wa¬likuwa chachu ya mafanikio ya Simba kwa msimu uliopita na kuchangia timu hiyo kutwaa ub¬ingwa wao wa 18.

Mvuto wa wachezaji hao ambao kwa umoja wao walifunga mabao 34 kati ya 62 yaliyofungwa na Simba kwa msimu mzima, uliwafanya mashabiki wengi kuingia uwanjani kuan¬galia mechi 30 za timu hiyo kwa msimu uliopita ambapo walishinda michezo 20 kati ya 30 na kutoka sare mechi tisa. Mechi moja pekee ndiyo walipoteza mbele ya Kagera Sugar.

Kwa mujibu wa takwimu za mapato kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara kutoka Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Simba waliku¬sanya jumla ya Sh 380,867,592 kwa msimu mzima huku wapinzani wao Yanga wakishika nafasi ya pili kwa kukusanya Sh 257,113,365.

Lipuli FC ya Iringa yenyewe iliingiza Sh 71,908,665 na kushika nafasi ya tatu, Singida United iliingiza Sh 68, 939,621 na kushika nafasi ya nne.

Nafasi ya tano, imeshikwa na Mbeya City ikiwa imeingiza Sh 54,766,008, Mbao FC ya sita Sh 51,719,270. Saba ni Majimaji Sh 49,377,409, nane Azam FC Sh 45,286,214, tisa Ndanda Sh 42,951,351, kumi Kagera Sugar Sh 40, 756, 536.

Njombe Mji ya 11 Sh 40,637,642, Stand United ya 12 Sh 36,126,778, Mtibwa Sugar ya 13 Sh 33,557,913, Prisons ya 14 Sh 28,580,829, Ruvu Shooting ya 15 Sh 19,774,569 na Mwadui FC ya mwisho Sh 19,135,116.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad