Otile Brown Alalamika Baada ya Kushutumiwa Kutumia Uchawi Kumteka Mrembo Vera Sidika


- Otile Brown mwenye ghadhabu aliwakaripia wanawake wenye kijicho mitandaoni

- Mwimbaji huyo alilalamika kwamba alikuwa akishutumiwa dhidi ya kutumia uchawi kumweka Vera

- Aliropokwa cheche za maneno makali akiwaanika wanawake kwa kudai ilikuwa jambo lisilowezekana kwa Vera kumpenda mtu wa kawaida Unapomchumbia sosholaiti, ni sharti uwe tayari kukumbana na kila aina ya matokeo yanayoambatana na kitendo hicho, na Otile Brown anajifunza taratibu faida na hasara ya kuwa mpenziwe wa kuhusudiwa Vera Sidika.

Uhusiano huo usiotarajiwa kabisa yamkini unanawiri kila uchao lakini hili halijawakomesha wakosoaji kupima mapenzi haya kuhusu ni jinsi gani mwanamziki kutoka kijiji kidogo pwani angeweza kumnyakua mwanamke aliye mfano mwafaka Kenya wa umbo kamilifu.

Hapo awali, ni Otile Brown aliyenyeshewa na maoni ya husuda ambayo yalipakiwa kama huruma kutoka kwa mashabiki na hata watu maarufu, huku wakidai alikuwa amepotea njia kwa kuamua kujaribu mambo na mwanamke ambaye sifa yake ilimsaliti kabisa. 

Otile hakufa moyo na akaendelea na ndoto zake za kuwa mpenzi ikiwemo kutoa kibao kwa jina huku akijitahidi kumwonyesha sosholaiti huyo alimaanisha mambo.

Maadamu yamkini msimamo wa Otile hautatikiswa na aina yoyote ya shutma, yaonekana sasa mahasidi wamebadili na nakala na sasa wanahisi ni Vera anayeelekea kuvunjika moyo mno hatimaye.
Otile aliyepandwa na ghadhabu alijitosa katika mtandao wa kijamii katika hatua isiyotarajiwa kulalamikia jumbe ambazo amekuwa akipo 

Otile, ambaye kwa kawaida huwa jasiri mno mitandaoni, aliwasuta wanawake ambao alidai wamekuwa wakisema aligeukia uchawi ili kuhakikisha Vera mwenye umbo la kudondosha mate hakumponyoka. Katika malamishi hayo  mahasidi wa Otile, ambao kwa namna ya kushangaza ni wanawake,wanadai mwanamme wa hadhi yake kifedha hangemudu kumweka Vera kupitia tu vitendo vya mapenzi na maneno matamu.

“Hivyo wasichana wamekuwa wakimtumia mpenzi wangu jumbe wakisema amefeli vibaya kwa kunipenda. Sisi husoma tu hizo jumbe pamoja (na Vera) na kucheka. Hivyo mmoja alinitumia ujumbe na ukanikwaza kwa sababu ulisema nilikuwa natumia hirizi kwake na hakuna vile Vera angempenda mwanamme wa kawaida kama mimi,” kilisema kijisehemu cha ujumbe wake.  

 "Kwa vile tu mwanamme hana hela za kununua mwilio wako haimaanishi ni mjinga. Ni werevu mno kukushinda. Sina muda wa kukuthibitishia chochote. Ikiwa ni sharti ujinadi ili ujenge himaya sitowahi kamwe kukuhukumu hadi utakapoanza kuwavunjia watu heshima,” alisema.  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad