Ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja hadi kumalizika kwa michuano hii mikubwa kabisa ya Kombe la Dunia pia ikisheheni vijana wadogo wenye ndoto za kufika mbali kisoka timu ya taifa ya Ufaransa hapo jana ilifanikiwa kutwaa taji la michuano ya kombe la Dunia kwa mara ya pili katika historia ya michuno hii baada ya kuifunga timu ya Croatia kwa mabao 4-2
Ufaransa wamefanikiwa kutwaa taji hili kwa mara ya pili baada ya miaka 20 wamefanikiwa kutwaa taji hili chini ya kocha mzawa Didier Deschamps amabye kwa upande wake ni mara yake ya pili kunyanyua kombe hili baada ya mwaka 1998 akiwa kama kapteni wa timu hiyo walifanikiwa kulitwaa taji hili kwa mara ya kwanza katika ardhi ya nyumbani lakini awamu hii amalinyanyua kama kocha na si mchezaji.
Ufaransa wamefanikiwa kutwaa taji hili wakiwa wamesheheni wachezaji wenye asili ya kiafrika 15 kati ya wachezaji 23,na hii ndo imekuwa sababu ya watu wengi Duniani kuwaonyeshea dalili za ubaguzi kwa kudai kuwa hawa siopraia wa Ufaransa.kitendo hiki kimekemewa vikali na Mwanamziki kutoka nchini Marekani P Didy kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweza kupost ujumbe ulioandikwa na Bwana Khaled Beydoun.
Bwana Khaled Beydoun ameweza kuwapongeza Ufarasa na kusema timu hiyo imeundwa na wachezaji wengi weusi pia wengi ni Waislamu lakini wametupilia mbali tofauti hizo za kidini na za kirangi wameweza kushirikiana na kuweza kupata ushindi kwa maana hiyo Waafrika na Waislamu ndio walioisaidia Ufaransa kutwaa taji hilo.