Picha za Utupu Zawaponza Irene Uwoya na Mobetto Waitwa TCRA.... Wapewa Onyo Kali

Msanii Irene Uwoya  na Mwanamitindo Hamissa Mobetto wamewajibishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA  kwa kosa la kuweka picha za Nusu uchi mitandaoni kinyume na kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2018.

Katika maamuzi yake na kwa kuzingatia utetezi wa Hamissa Mobetto ambaye amesema picha hizo alizipiga mwaka jana nchini Kenya, TCRA  imempa Onyo la mwisho na kwamba akirudia, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, TCRA imemtaka Hamissa Mobetto kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram la kuwaomba msamaha watanzania na kuwataka kutosambaza picha zake za nusu uchi.

Kwa upande wa Irene uwoya, yeye pia kapewa Onyo la mwisho kwa kuzingatia utetezi wake alioutoa, pia ametakiwa kuomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Baada ya kusomewa makaosa yake Hamisa Mobeto alianza kwa kuishukuru TCRA na kukiri kosa huku akidai kuwa katika kutafuta maisha kwa vijana kunakuwa na njia nyingi na aliahidi kuwa barozi mzuri kwa kutoa elimu juu ya sheria hiyo kwa wanamitindo wenzake na wale wanaopata dili kama yeye za kupiga picha.

"Nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa aliokwazika na picha zangu na nahaidi kuwa balozi mzuri kwa wanamitindo kama mimi au waliokuwa wanapiga picha kama mimi najua watu wengi hawana  elimu ya kutosha kuhusiana na sheria hii mpya nahaidi  nitakuwa barozi ili nao wasije kuitwa kama mimi huku" alisema Hamisa.

Naye Irene uwoya aeiomba TCRA kutoa kuandaa semina na kutoa elimu kwa wasanii kwakuwa wengi wao hawajui hiyo sheria.

"Nashukuru kwa kuongea na sisi kama wazazi maana nnilivyoitwa sikutegemea kama itakuwa hivi  sababu nilikuwa nawaza tofauti nashukuru kwa kuongea nanyi naomba radhi kwa kuposti picha niliyoiposti ombi langu kwenu tungeitwa wasanii wate na kuelimishwa ili mtu atakapofanya ajulikane kuwa amefanya makusudi" alisema Uwoya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad