Bodi ya michezo ya kubahatisha imetekeza kwa moto mashine feki 12 za mchezo huo ambazo zimekamatwa katika wilaya za rombo, moshi vijijini na manspaa ya moshi mkoani kilimanjaro baada ya kuiangizwa nchini visivyo halali.
Meneja wa Ukaguzi na Udhibiti wa Bodi hiyo Sadiki Elimsu amesema, wamiliki wa mashine hizo zenye thamani ya shs. 24mil/= ambazo pia hazina viwango wametoroka na juhudi zinafanywa na jeshi la polisi mkoani kilimanjaro za kuwatia mbaroni.
Elimsu amesema, wamiliki wa mashine hizo pia walikuwa wakiichezesha mchezo huo bila kulipia kodi na kuikosesha serikali mapato ya zaidi ya shs. 100mil/= kwa mwaka mmoja uliopita.
Kamanda wa polisi mkoani kilimanjaro kamishna msaidizi wa polisi Hamisi Issa amesema, jeshi la polisi limeanzisha msako mkali wa kuwatafuta wamiliki hao ambao wanafahamika ili wafikishwe mahakamani kwa kuingiza mashine hizo kinyemela na kuikosesha mapato serikali.