Polisi Kilimanjaro yaanzisha msako wa mashine feki


Bodi ya michezo ya kubahatisha imetekeza kwa moto mashine feki 12 za mchezo huo ambazo zimekamatwa katika wilaya za rombo, moshi vijijini na manspaa ya moshi mkoani kilimanjaro baada ya kuiangizwa nchini visivyo halali. 

Meneja wa Ukaguzi na Udhibiti wa Bodi hiyo Sadiki  Elimsu amesema, wamiliki  wa mashine hizo zenye thamani ya shs. 24mil/=  ambazo pia hazina viwango  wametoroka  na juhudi zinafanywa na jeshi la polisi mkoani kilimanjaro za  kuwatia mbaroni. 

Elimsu amesema, wamiliki wa mashine hizo pia  walikuwa wakiichezesha mchezo huo bila kulipia kodi na kuikosesha serikali mapato ya zaidi ya shs. 100mil/= kwa mwaka mmoja uliopita. 

Kamanda wa polisi mkoani kilimanjaro kamishna msaidizi wa polisi Hamisi Issa amesema, jeshi la polisi limeanzisha msako mkali wa kuwatafuta wamiliki hao ambao wanafahamika ili wafikishwe mahakamani kwa kuingiza mashine hizo kinyemela na kuikosesha mapato serikali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad