Polisi Nchini Ethiopia Yalaumiwa kwa Kuwatesa na Kuwabaka Wafungwa

Polisi Nchini Ethiopia Yalaumiwa kwa Kuwatesa na Kuwabaka Wafungwa
Maafisa wa Polisi nchini Ethiopia wamelaumiwa kwa kuwatesa kwa vipigo na kuwabaka wafungwa wa kike, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa na shirika la kutetea haki za binadamu ‘Human Right Watch’ kuonesha kuwa wafungwa wa kisiasa walivyobakwa katika jimbo la Somalia.

Ripoti hiyo imewashutumu maafisa wanaofanya kazi katika jela ya Ogaden pamoja na maafisa wa kikosi cha Polisi cha Liyu, kwa kuwapiga na kuwabaka wafungwa wa kike wanaodaiwa kuwa waasi wa kundi la upinzani la Ogaden Liberation Front.

Human Right Watch ili wahoji wafungwa zaidi ya 100 waliokuwa wamefungwa katika gereza la Ogaden kati ya mwaka ya 2011 na 2018 huku wafungwa hao wakikaririwa kuwa walivuliwa nguo na maafisa wa gereza hilo kisha kubakwa.

Aidha katika ripoti hiyo imeonesha kuwa watoto wengi wamezaliwa kwa njia ya ubakaji huku wakiwa ndani ya 'seli' vyumba vya wafungwa bila huduma za kiafya.

Hata hivyo Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed, amekiri kuwa maafisa wa usalama wamewatesa wafungwa hao na serikali itafuatilia suala hilo na wote waliohusika watawajibishwa kisheria.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad