Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM limemkamata Amin Kimario (55) mkazi wa Manzese na wenzake watatu kwa kosa la wizi wa kughushi hundi za benki mbalimbali na kuziweka kwenye akaunti za washirika wake.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya DSM, Rebaratus Sabas amesema watuhumiwa hao wamekamatwa June 24, 2018 huko Kariakoo ambao katika mahojiano na Jeshi la Polisi walikiri kujihusisha na uhalifu huo na walieleza kuwa wamekuwa wakighushi hundi za benki tofauti kisha kuziweka katika akaunti ya benki ili kufanikiwa kuiba fedha walizokusudia.
Sambamba na wahalifu hao Jeshi la Polisi linashikilia gari aina ya Toyota IST namba T 819 DED iliyokuwa ikitumiwa na wahalifu hao, simu za mkononi 8, kadi za simu 6 za mitandao mbalimbali, pamoja na deposit slip ya Tsh 1,973,750 ya hundi ya NMB kwa uchunguzi zaidi.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Omwailimu Binyakusha anayemiliki kampuni inayoitwa Arise Special Sunrise Safaris ambaye kwa tuhuma za kutapeli watalii wawili, mmoja anaishi Marekani na mwingine anaishi India (ni mtu na mama yake).
Mtuhumiwa alichukua kiasi cha Dola za Kimarekani 5000 na kushindwa kuwapeleka safari walizokubaliana ambapo mtuhumiwa aliamua kuwatelekeza wageni hao hadi walipohudumiwa na serikali.