Rais JPM Ampa Milioni 10 Wakonta Kapunda

Rais JPM Ampa Milioni 10 Wakonta Kapunda
Rais Dkt. John Magufuli amempatia msaada wa Tsh. Milioni 10, binti Wakonta Kapunda mwenye ulemavu wa miguu na mikono anayeandika kwa kutumia ulimi, ili zimsaidie kutimiza ndoto yake ya kuwa mwongozaji wa filamu (film director).



Magufuli ametoa pesa hizo leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Ukumbi wa Serena Hotel jijini dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha mfanyabiashara Dkt. Reginald Mengi kinahoitwa ‘I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success’ chenye maudhui ya kumfundisha Mtanzania kujikwamua kutoka kwenye umaskini.



Mbali na Magufuli, Mzee Mengi pia amempatia binti huyo kiasi cha dola 20,000 (sawa na Tsh. Milioni 45.45) kutokana na kuandika andiko bora la biashara ambapo Mzee Mengi huwasaidia vijana wa Kitanzania wanaoweza kuandika na kutekeleza andiko zuri la kibiashara ili waweze kuondokana na umaskini.



Wakonta alipata ajali na wanafunzi wenzake wa Kidato cha sita katika, Shule ya Sekondari Wasichana Korogwe, mkoani Tanga mwaka 2012 na kumsababishia ulemavu huo, lakini hakukata tamaa amekuwa akipambana ili aweze kutimiza ndoto zake, na leo njia imeanza kuonekana baada ya kupokea msaada huo ambao ni jumla ya ya Tsh. Milioni 55.45.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad