Rais Magufuli amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na WFP hasa katika kukabiliana na changamoto ya wakulima kukosa soko la mazao ya ziada na amebainisha kuwa katika msimu huu Tanzania ina takribani tani Milioni 4 za chakula cha ziada kinachopaswa kuuzwa nje ya nchi.
“Namshukuru sana kwa kuunga mkono juhudi tunazozifanya kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na hii ndio njia pekee ya kuhakikisha nchi inajikomboa kwa kuwa na uchumi wa kweli” Rais Magufuli
“Tumedhamiria kujitegemea na pia namshukuru kwa kuunga mkono ‘Hapa Kazi Tu’ na juhudi zingine zote ikiwemo kupambana na rushwa na kwamba anaiona Tanzania ya pekee na yenye mwelekeo tofauti wa kuleta neema” amesema Rais Magufuli.