Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema ili kuepuka chuki, vurugu na mafarakano katika taifa, viongozi wa dini wanatakiwa kujiepusha na kukejeli dini ama dhebu lingine wakati wote wanapotekeleza majukumu yao wasiruhusu siasa kuingilia majukumu ya dini.
Dkt. Magufuli amesema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Muhagama, wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu askofu mteule Ezekiel Yona wa kanisa la Monravian jimbo la Magharibu Mkoani Tabora.
Waziri Mhagama amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia katiba ya nchi ili kila dhehebu na waumini wa madhahebu mbalimbali waweze kuabudu bila shida yoyote.
Kwa habari kamili msikilize hapa chini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Muhagama akielezea zaidi.