Rais John Magufuli amemuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi wa kujenga daraja kubwa la Selander Bridge kutoka Coco Beach mpaka Agha Khan litakalogharimu shilingi bilioni 250 kwa ufadhili wa Serikali ya Korea kusini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ndani ya miezi 36 aliyopangiwa kufanya kazi.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kushuhudia mkataba wa utiaji saini ujenzi wa darala hilo ambalo litakuwa na urefu wa kilomita 6.23 mbele ya Waziri Mkuu wa Korea Kusini Mh.0 Lee Nak-Y eon Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kukamilika kwa daraja hilo kutaendelea kubadilisha taswira mpya ya Jiji la Dar es Salaam katika miundombinu ya barabara.
Katika tukio jingine, hivi sasa Rais Magufuli anapokea gawio la kipindi cha mwaka 2017/18 kutoka Wakala, Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma 47 ambayo Serikali inamiliki hisa.