Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kutembelea ukumbi wa starehe mjini Lagos Nigeria unaomilikiwa na nguli wa muziki ( Afro beat) kutoka Nigeria, Fela Kuti na kuwa Rais wa kwanza kuingia katika ukumbi huo maarufu kwa watumiaji wa marijuana, wacheza uchi na kamari.
Rais Macron baada ya mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika jumapili katika mji mkuu wa Mauritania (Nouakchott ) anatarajiwa kuelekea Abuja Nigeria ambapo atakutana na mwenyeji wake Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na kuzungumzia suala la usalama na mpango wa kupambana na ugaidi.
Aidha Rais Emmanuel Macron baada ya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Buhari atahudhuria mkutano wa wanamitindo kutoka maeneo tofauti Afrika na waigizaji wa Nollywood utakaofanyika katika ukumbi huo wa starehe (Casino).
Mwakilishi wa taasisi ya utamaduni mjini Lagos Ibrahim Tcha-Tchere amesema kuwa lengo kuu la Rais Macron ni mpango wa kuanzisha mahusiano mapya kati ya Ufaransa na Nigeria kuhusu utamaduni.