Rais wa zamani wa Club ya Barcelona ashutumiwa kumnunulia Abidal ini la magendo

Rais wa zamani wa Club ya Barcelona ashutumiwa kumnunulia Abidal ini la magendo
Leo July 4,2018 nakuletea stori hii kutoka huko nchini Hispania ambapo unaambiwa kuwa kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa Rais wa zamani wa Club ya Barcelona Sandro Rossell alimnunulia ini kwa njia ya magendo beki wake Eric Abidal mwaka 2012.

Hata hivyo taarifa hiyo imepingwa vikali na Barcelona pamoja na Abidal mwenyewe ambaye kwa sasa ndie Katibu wa Club hiyo.

Mwaka 2012 beki Raia Ufaransa Abidal alisumbuliwa na tatizo la ini lililomlazimu kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kumpandikizia ini jingine ambalo ndilo linalodaiwa kununuliwa kwa njia ambazo sio halali Rais huyo wa zamani wa Barcelona.

Aidha Shirika la upandikizaji wa viungo vya ndani ya mwili nchini hispania limeanzisha uchunguzi wa ndani likishirikiana na hospitali husika na shirika la upandikizaji la eneo la Catalan kubaini ukweli wa sakata hilo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad