Rally alimtaja mamaye Diamond kama mkewe huku akiadhimisha siku ya kuzaliwa


- Rally alimtaja mamaye Diamond kama mkewe huku akiadhimisha siku ya kuzaliwa

- Kauli yake iliwaacha wengi na maswali wengine wakishangaa iwapo alikuwa amefunga pingu za maisha na mamaye Diamond

Rally Jones, mpenzi wa mamaye msanii wa Tanzania Diamond Platinumz, Sandrah amewaacha wengi vinywa wazi kwa kumtaja kama mkewe.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Instagram, Rally ambaye amejulikana kama mpenziwe Sandrah aliichapisha picha akiwa amemshika mkono mamaye Diamond na kubainisha jinsi alivyojawa furaha kuhusu uhusiano wao.

Wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapoenzi kwa muda. Picha: Iamrallyjones/Instagram

Rally alitayafanya matangazo hayo Jumamosi, Julai 7 huku akimtakia Sandra heri njema akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

‘’ Nafurahi sana kuwa na mwanamke spesheli kama huyu maishanai mwangu. Noamba Mungu akujalie maisha marefu. Happy Birthda mke wangu mama Dangote. Nakupenda,’’ aliandika.

Rally Jones alieleza kuwa alikuwa na furaha kuwa naye. Picha: Iamrallyjones/Instagram Source: Instagram

Kauli ya Rally inajiri miezi michache baada ya wawili hao kukiri kuwa walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

Uhusuano wao uliibua hisia kali awali, wengi wakidai kuwa mamaye Diamond aamemzidi Rally umri.

Licha ya kukashifiwa vikali, walijitia hamnazo na kuendelea na uhusiano wao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad