Rapa Mwingine Aiawa Kwa Risasi Marekani, ni Rafiki wa Damu wa Drake


Ikiwa zimepita siku mbili tu tangu Rapa Drake aachie album yake mpya ya Scorpion, mkali huyo kutoka Canada usiku wa kuamkia leo amepatwa na msiba mzito wa rafiki yake mkubwa nchini Canada ambaye pia ni rapa aitwaye Smoke Dawg. 

Imeelezwa kuwa rapa Smoke Dowg amepigwa risasi na watu wasiojulikana kwenye vurugu jijini Toronto na tayari Drake kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibisha taarifa hizo. 

Ukaribu wa Rapa Smoke Dawg na Drake ulianza mwaka jana baada ya Rapa  kujizolea umaarufu nchini Canada kwa kufanya remix ya wimbo wa Trap House ya French Montana. Tazama video ya wimbo wake wa mwisho alioutoa wiki iliyopita. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad