Ratiba ya Ligi Kuu Yatoka Simba na Yanga Kukutana na Yanga

Ratiba ya Ligi Kuu Yatoka Simba na Yanga Kukutana na Yanga
Pazia la ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2018/19 litafunguliwa rasmi Agosti 22 kwa jumla ya timu 12 kushuka dimbani kukamilisha mechi 6 za ufunguzi ambapo mabingwa watetezi Simba watacheza na Tanzania Prison kwenye uwanja wa taifa.


Yanga itaanzia ugenini huko Morogoro Agosti 23 kucheza na timu ya Mtibwa Sugar huku Azam FC wakianza nyumbani kukipiga na Mbeya City.  Ratiba hiyo inaonesha pambano la watani wa jadi litapigwa Septemba 20 kwenye uwanja wa taifa na Simba watakuwa wenyeji wa Yanga.

Kwa upande wa timu zilizopanda ligi kuu msimu huu Alliance watacheza na Mbao FC, Biashara United wakianza na Singida United. JKT Tanzania watakipiga na KMC, African Lyon watacheza na Stand United huku Coastal Union wakicheza na Lipuli FC.

Aidha Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amesema mechi ya Ngao ya Jamii kati ya bingwa Simba na bingwa wa kombe la shirikisho Mtibwa Sugar itapigwa Agosti 18 kwenye uwanja wa CCM Kriumba Mwanza.

Msimu huu utashirikisha jumla ya timu 20 kutoka 16 zilizoshiriki msimu uliopita. Timu tatu zitakazoshika nafasi za chini moja itashuka moja kwa moja huku mbili zikicheza mechi na washindi wa pili na tatu wa ligi daraja la kwanza na wakifungwa wanashuka ila wakishinda wanabaki ligi kuu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad