Ray c Alizwa na Maisha ya Uokovu ya Lulu Michael


Mwanadada Ray c amefunguka katika ukurasa wake wa instagram baada ya kuona video ya lulu michael inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Lulu akiwa kanisani anaimba kwaya na kusema kuwa video hiyo imemkumbusha mbali sana hasa kipindi yeye alipokuwa hoi akiumwa alikuwa akimkumbuka sana mungu lakini baada ya kupona amemsahau Mungu kabisa.

Baada ya kuiona video hiyo Ray c aliandika
“Lulu nimeangalia video hii zaidi ya mara kumi nahisi lakini mpaka machozi yamenilenga kabisa,sikumbuki ni lini nimeingia kanisani tena.najiona mzima sasa na kumsahau kabisa mungu wangu , najifunza kitu kutoka kwako my dear.you inspire me.

Video hiyo ya lulu iliyomuonyesha akiwa kanisani akiimba na kuabudu iliwafurahisha watu wengi ukizingatia kwamba kwa muda mrefu Lulu alikuwa haonkani katika mitandao ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad