Ray C Amuunga Mkono Muna "Naamini Kuna Mzigo wa Maumivu Kutoka Moyoni Mwako Umeutua"

Ray C Amuunga Mkono Muna "Naamini Kuna Mzigo wa Maumivu Kutoka Moyoni Mwako Umeutua"
Baada ya muna kuongea yaliyopo moyoni mwake kuhusu swala la marehemu mtoto wake Patrick   kusema wazi juu ya baba wa mtoto wake kuna watu waliongea mengi kila mtu akim-judge  Muna kwa lake huku wengine wakisema kuwa ameyafanya mapema sana mambo hayo alitakiwa kusubiri mpaka 40 ya mtoto huyo  ipite ndio aongee hayo.

Lakini wapo waliomtetea na kumuona kama alichokifanya labda kinaweza kumsaidia kukaa kwa amani lakini pia labda kingeweza kufunga midomo ya baadhi ya watu waliokuwa wakimhukumu bila kujua kwa nini yalitokea yaliyotokea.

Ray c ameguswa na maamuzi ya Muna na hivyo aliamua kuongea kuhusu swala hilo la kumpongeza kwa kumwambia kuwa aloichokifanya kimeweza kumuondolea mzigo wa maumivu yake aliyokuwa nayo kuhusu mtoto wake.

"Una uhuru wa kuwa muwazi pale unapoona mambo fulani yamekuumiza au hayajakaa sawa,kuongea kuna kufanya nafsi yako inakaa sawa,safi muna ninaamini kuna kamzigi flani umekatua  kutoka kwenye moyo…good job.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad