RC Makonda Asitisha Usafi Kila Jumamosi

RC Makonda Asitisha Usafi Kila Jumamosi
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametangaza rasmi kuondolewa kwa  kipengele kilichokuwa kikiwataka wafanyabiashara kufunga maduka siku Jumamosi hadi Saa nne asubuhi kwaajili ya usafi na badala yake jukumu amelikabidhi kwa zaidi ya Vijana 4,000 wa JKT.


Makonda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Vijana wa JKT na Mgambo, waliojitokeza katika usaili wa kuajiriwa ili kusimamia zoezi la usafi na kuhakikisha wanawawajibisha wanaochafua mazingira jijini, huku wafanyabiashara wakifungua maduka yao kama kawaida.

“ Wafanyabiashara kufunga maduka yao siku ya Jumamosi hadi Saa nne asubuhi, hilo halitakuwepo tena na badala yake nawakabidhi jukumu hilo na atakayekaidi zoezi la Usafi na kutupa taka ovyo akamatwe maramoja”, amesema Makonda.

Aidha Makonda amesema vijana hao watakuwa na jukumu la Kusimamia kampuni zilizopewa kazi ya Usafi kwenye maeneo husika, Kuwakamata, kuwatoza faini watupaji wa taka pamoja na kufuatilia kujua kila nyumba inapeleka wapi taka wanazozalisha ambapo ifikapo Jumanne ya Julai 10 itakuwa ndio mwisho wa usajili wa vijana hao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad