Rekodi zinasemaje kuhusu Ufaransa vs Croatia? Wote wana nafasi

 
Wakati watu wengi wakiwaza ni ajabu kwa Croatia kwenda fainali na huku wana watu milioni 4.17 tu nchini mwao, wanasahu mwaka 1930 ambapo Uruguay walikwenda fainali huku taifa lao likiwa na watu milioni 1.7 na wakabeba ubingwa.

Mwaka 1991 ndipo taifa hili lilipata uhuru wake kamili, na raia wa Croatia wanaamini kuingia katika fainali za mwaka huu ni kama ndoto kwao ambayo imetimia wakiwa na imani wanaweza fanya lolote dhidi ya Ufaransa.

Kuna wazee wanaoamini kuhusu data na rekodi na wanaoamini hivyo wanawapa Croatia nafasi kubeba kombe hii leo kwani mara mbili zilizopita ambazo taifa lilicheza fainali ya kombe la dunia ya kwanza kama ilivyo Croatia walibeba kombe hilo(Ufaransa 1998 na Hispania 2010).

Lakini Croatia wakiwaza hivyo, kwa Ufaransa mawazo yao ni tofauti na matumaini yao ni makubwa sana hii leo kwani hawa Wacroatia wameshawafunga katika mara zote tano ambazo timu hizi zimekutana.

Mwaka 1998 ngoja nkukumbushe, Croatia walikutana na Ufaransa katika mchezo wa nusu fainali kombe la duniana Croatia wakaanza kufunga wao lakini baadae Ufaransa walisawazisha na wakapata goli la ushindi mechi ikaisha 2-1.

Endapo Ufaransa watafanikiwa kubeba kombe hii leo baasi Didier Dechamps atakuwa kocha wa tatu kuwahi kuchukua kombe hilo kama mchezaji na pia kocha baada ya Mario Zagallo na Franz Bckenbauer.

Kylian Mbappe atavunja rekodi nyingine ya Pele hii leo kama atafanikiwa kufunga goli kwani atakuwa kinda wa pili kuwahi kufunga katika fainali za kombe la dunia tangu baada ya Pele kufunga mwaka 1958.

Ufaransa pia wanatafuta nafasi hii leo ya kuingia kwenye kundi la mataifa ambayo yamebeba kombe hili zaidi ya mara moja wakiungana na Brazil, Ujerumani, Italia na Argentina.

Shafih Dauda
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad