“MWAKA 2010 nilitoa wimbo wangu wa kwanza wa Uzuri Wako, kazi hii ilikuwa ina vikwazo vingi sana ila tukafanikisha lokesheni, lakini msanii niliyefanya naye kazi sikumpata kwa muda na aliyesaidia hili alikuwa rafiki yangu Rama na mwenzake HK haikuwa rahisi kabisa kama tunavyoiona na mpaka kumpata video queen niliyekuwa natamani kufanya naye kazi kwa wakati huo alikuwa wa moto sana anaitwa Lulu (Elizabeth Michael).
“Usichokijua kwenye hii video, ndoto yangu kubwa nilitaka kufanya na Adam Juma suala hili lilikuwa gumu kwa kipindi hicho, kipato kilikuwa kidogo ikabidi Adam atupe mtu anaitwa Mejja ambaye alikuwa Visual Lab hapohapo tukashukuru ila mimi moyo wangu nilitamani sana Adamu Juma kwani ndo ilikuwa ndoto yangu kubwa kufanya naye kazi.
“Sikuchoka kujitahidi hatimaye video yangu ya Silali nikafanya na Adam Juma, pia kazi hii ilikuwa na matatizo mengi ambayo kiubinadamu sipaswi ya sema namshukuru sana Adam alilimaliza suala hili likawa limekaa sawa…ninachotaka kusema hapa ni kwamba safari yangu ya kufanya video ni ni funzo kwa vijana ambao wanatamani kuwa wasanii wa muziki huu una VIKWAZO.
“Usije ukawa mtu wa kulalamika maana kumbuka hivi vitu haviji kirahisi kudharaulika ni kawaida sana, tena usije ukasusa maana haitukusaidia kaza mana safari yake kuna mawili kupata au kukosa ila moyoni mwake jiwekee kupata ili uwe na moyo hata pale unapokosea kwamba ufanye kwa bidii ipo siku kuchoka kwenye kazi hii ni mwiko. Pia ni kazi ambayo inahitaji uwe mpole sana mana kila mtu atatamani kukuelezea tofauti mara unaringa palePicha inayohusiana
unapoonekana unapata so ishi nao vizuri jaribu hata kujishusha ishi kama bwege na kuheshimu hata kitu kidogo ambacho unaambiwa ingawa muda mwingine unaona kabisa hichi siyo ila sikiliza maana kwenye maneno kumi utakayoambiwa huenda kuna ukweli hata robo au nusu.”
Najaribu kukumbusha tu baadhi ya maneno ambayo Rich Mavoko aliwahi kuyaweka mtandaoni siku chache baada ya kusainiwa na Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Mavoko ambaye jina lake la kuzaliwa ni Richard Martin ni miongoni mwa wasanii wakali kuwahi kutokea katika muziki wa Bongo Fleva, ana nyimbo nzuri, ni mtunzi mahiri wa mashairi na pia ana sikio la kumrekebisha prodyuza.
Jaribu kutega sikio kwenye ngoma zake kama vile Silali, Follow Me, Wanakutamani, Uzuri Wako, Sheri, Rudi, Roho Yangu, Kokoro kisha nifuate kwa hoja! Uwezo wa Mavoko ulikuwa juu na wengi walikuwa wakifananisha levo zake sawa na wakali wengine kama vile Alikiba na Diamond.
June 2, 2016, Mavoko alitambulishwa rasmi ndani ya Lebo ya WCB na kuungana na Harmonize na Rayvanny kipindi hicho. Mengi yaliong-elewa kuingia kwake huko huku wengine wakienda mbali zaidi na kumuona kama anajic-himbia kaburi lake mwenyewe. Miaka miwili sasa imekatika, Mavoko hajawika kivile ndani ya WCB kama ilivyokuwa kwa wasanii wenzake, Harmonize na Rayvanny. Mara nyingi ameonekana kama kuwa nyuma ya wasanii hao hususan katika mpangilio wa kutoa kazi mpya.
MAVOKO AMEJITOA?
Tetesi za ‘town’ ni kwamba Mavoko amejitoa ndani ya WCB, vipo viashiria vinavyoweka wazi kuwa hayupo na lebo hiyo; la kwanza, kwa sasa Mavoko ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Happy. Kama ilivyo kwa wasanii wote wa WCB, kuanzia audio huwa una viashiria kuwa yupo lebo hiyo lakini hakuna.
Pili, msimamizi wake mkuu, Diamond Platnumz amekuwa karibu na Mavoko pindi anapoachia kazi mpya’ lakini hadi sasa hakuna sapoti yoyote inayoonekana na hiyo inadhihirisha kuwa hawapo vizuri. Tatu, video aliyoachia nayo kama ilivyo kwenye audio, haina viashiria vya kuonesha imesimamiwa na WCB.Tokeo la picha la RICH MAVOKO
MAVOKO ANASEMAJE?
Showbiz lilimtafuta Mavoko kujua ukweli wa hili ambapo alionesha ‘kuwaka’ juu ya ukweli.“Siwezi kuongea lolote kwa sasa labda utafutwe uongozi wa WCB ndo unaweza kuongelea hili.”
BABU TALE ANENA
Upande wa Meneja wa WCB, Babu Tale naye alitafutwa kujua hili alisema WCB kuna utaratibu wa kuachiana nafasi na kwa Mavoko ndiye aliyekuwa anafuata. “Sioni haja ya kuongopa kwamba hayupo WCB, kwa sababu hata asipokuwepo lazima itajulika tu kwa watu kwamba hayupo, Mavoko yupo ila wakati yanatokea haya yote alikuwa na matatizo yake, pia alikuwa bize anashuti nyimbo zake.”
WENGINE LIPOJE HILI
Ipo ‘theory’ kuwa wanamuziki wote wanaong’ara chini ya mwamvuli wa staa huwa hawakui. Rejea msanii Mayokhoun na Bred ambao walikuwa wakali lakini wakawa chini ya Davido hadi leo hawajulikani walipo. Yuko wapi Corede Bello, kinda wa Don Jazz? Hata Tekno kama siyo kushtukia kujitoa kwa Davido asingekuwa staa mkubwa Afrika. Rudi Bongo, tupa jicho lako kwa Barakah The Prince aliyekuwa chini ya Kiba, Neddy chini ya Dimpoz au nenda Congo DR waone Fally Ipupa na Fere Gora waliokuwa chini ya Koffi Olomide.
Imebaki Stori
Ikumb-ukwe wakati Mavoko anaingia WCB, wimbo wake wa kwanza ulikuwa imebaki stori na kichupa kilienda kutengenezewa Sauz ‘Afrika Kusini’ na sasa ameonesha wazi kuachana na lebo hiyo na vyote alivyovifanya kwao IMEBAKI STORI.
STORI: MEMORISE RICHARD
Rich Mavoko WCB, Haya Yanaonyesha Kuwa 'Imebaki Stori Imemrudia yeye Mwenyewe'
0
July 27, 2018
Tags