Roboti Sophia Afanya Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia

Roboti Sophia amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia
Sophia ni roboti aliyepata umaarufu na kupewa uraia wa Saudi Arabia, kwa uwezo wake wa kuongea, kujibu maswali, ishara za uso, na kusoma hisia za watu anaoongea nao.

Amewasili bara la Afrika nchini Ethiopia kuonana na Waziri mkuu Abiy Ahmed siku ya jumatatu na kuongea kuhusu misaada ya ubunifu wa teknolojia. Ingawa alipata hitilafu kidogo ya vipande vya mwili wake kupotea Airport wiki iliyopita. Ikafikia hatua ya kuahirisha mkutano na chakula cha usiku na waziri mkuu ijumaa iliyopita.

Sophia atahudhuria maonyesho ya ICT yaliyo anza kuonyesha jumatatu nchini humo Ethiopia.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad