Serikali imefunga migodi 2 ya dhahabu


MBEYA: Serikali imefunga migodi 2 ya dhahabu baada ya kubaini kuwa inaendesha shughuli zake bila kufuata sheria wala kanuni za mazingira

Migodi hiyo pia inaelezwa inahatarisha usalama wa mali na maisha ya wananchi katika kata ya kiwanja wilayani Chunya.

Migodi yote miwili mbali ya kuharibu mazingira pia imebainika kuwa haina cheti cha tathimin ya mazingira kutoka baraza la usimamizi wa mazingira NEMC

Pia migodi hiyo imegundulika kuwa haina cheti cha mamlaka ya usalama mahali pa kazi na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na mali za Watu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad