Shilole Angemuiga Diamond Angeongea Umombo Haraka Sana Ila Tatizo Lake Hili Hapa


By Luqman Maloto

MTAALAMU wa Kiingereza, Sarah Li Cain, raia wa Canada, ameshaandika makala nyingi kuelezea mbinu mbalimbali za kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha.

Hapa nimechagua andiko lake "How to Speak English With Confidence in 9 Easy Steps". Tafsiri yake ni jinsi ya kuzungumza Kiingereza kwa kujiamini katika hatua tisa rahisi. Katika hizo hatua tisa, nimependa kuizungumza ya tatu inayosema: "Make Friends with English Speaking Expats." Kwamba tengeneza urafiki na watu wenye umahiri wa kuzungumza Kiingereza.

Ukitaka kujua 'English Course' ya Diamond ndiyo hiyo namba tatu; kujenga urafiki na mafundi wa kuzungumza Kiingereza. Uzuri Diamond marafiki aliowatengeneza hawakuwa wa juujuu, bali ni wale ambao hata giza lilipoingia, alichangia nao shuka. Marafiki ambao alitumia muda wake mwingi pamoja naye.

Ndiyo, Diamond amekuwa hodari sana wa kuchagua wapenzi ambao ni mafundi wa kutafuna yai, tena yai lenyewe ni lenye kitunguu. Soma hii orodha; Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa 'Penny', Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady'. Unakuwa na wapenzi hao kwa nyakati tofauti halafu usijue Kiingereza si ni kurogwa huko?

Wema anafahamika kwa kutema ung'eng'e. Hawezi kuzungumza sentensi mbili bila Kiingereza. Jokate si mzungumzaji sana wa Kiingereza, ila ni hodari sana. Jokate ni msomi sana huyu mrembo. Penny, kwake ndipo mayai hutagiwa. Zari kwao Uganda mayai ndiyo hukaangwa. Lugha anazozifahamu vema ni Kiingereza na Kiganda, lakini huzungumza zaidi Kiingereza.

Kama Shilole naye angekuwa na orodha ya wapenzi wenye ufundi mzuri wa Kiingereza, bila shaka angekuwa anakizungumza sana. Maana Diamond hivi sasa ni fundi, ukimwita kwa ajili ya mahojiano ya Kiingereza hana shida. Ulimi unanyooka vema tu.

Shilole labda kwa sababu amekuwa na Nuhu Mziwanda ambaye naye minara ya Kiingereza haisomi na sasa ameshaolewa na Uchebe ambaye ni wazi hiyo lugha kwake bado inaleta usumbufu. Maana kama angekuwa na ufundi mdogo tu wa lugha ya Malkia, asingeshindwa kumfundisha mkewe kutamka neno 'subscribe', mpaka aende British Council.

Haimaanishi amwache Uchebe, ila tunamkumbusha kuwa mwenzake Diamond sasa hivi yupo mbali

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad