Shilole: Q Chief Ndiye Aliyegundua Kipaji Changu na Kunishawishi Kufanya Mziki

Shilole: Q Chief Ndiye Aliyegundua Kipaji Changu na Kunishawishi  Kufanya Mziki
Msanii wa Bongo Fleva Shilole amefunguka kuwa  mtu aliyemwambia  kuwa ana kipaji cha kuimba na kumshawishi  kufanya mziki ni Q Chief.

Akizungumza na www.eatv.tv shilole amesema yeye hakuwa anajua kama ana kipaji cha kuimba lakini alikuwa anatamani tu japo alikuwa anaamini kuigiza ndio mahali pake.

Shilole amesema alikuwa anatamani ila hakujua ataanzia wapi lakini alipokutana na Q Chief alimuambia anatamani kuwa muimbaji ndio ukawa mwanzo mzuri wa yeye kuingia studio, ni baada ya Q Chief kumwambia unaweza.

“Unaweza kuwa na kitu ndani yako ila usijue kama unaweza ila mimi sasa hivi nafanya vizuri kuliko nilivyokuwa kwenye Bongo movies na pia kwenye muziki niko huru sana kuliko nikiwa naagiza”,amesema Shilole.

Hata hivyo, Shilole ameongeza kwa kusema siku amesikia Q Chief ametangza kuacha muziki, aliumia kwakuwa anajua uwezo wake ni mkubwa na alikuwa anaona wanapoteza kipaji kikubwa katika tasinia ya muziki nchini.

“Ila sasa hivi naona raha baada ya kuona yeye kutengua kauli yake na kuendelea na muziki na nyimbo yake mpya naipenda halafu ni kali. Kwahiyo mimi ni jambo la kujivunia kwa kuona mtu ambaye alinigundua upande wa pili katika tasnia ya kuimba amerudi tena”,amesema shilole.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad