Shindano la wanaume kubeba wake zao lafanyika Finland


Mashindano ya Dunia ya Wanaume kuwabeba Wake zao yamefanyika nchini Finland ikiwa ni kwa mwaka wa 23 mfululizo. 

Katika mashindano hayo ambayo yamefanyika katika mji mdogo wa Sonkajarvi ambao una wakazi takribani 4,200 uliwahusisha wanaume ambao waliwabeba wake zao mabegani na kukimbia nao kwa mita kadhaa na kuhudhuriwa na mamia ya wageni toka pande mbalimbali. 

Jumla ya familia (mke na mume) 53 zilishiriki katika shindano hilo ambalo lilishirikisha nchi 13 zikiwemo Marekani, Uingereza, Estonia, Sweden na Lithuania. 

Wazo la kuanzisha shindano hilo lililetwa mnamo karne ya 19 na Ronkainen the Robber ambaye aliwashawishi vijana wenzake kubeba kati ya gunia la mbegu ama kumbeba nguruwe na kukimbia nae. 

Shindano hilo lilihusisha washiriki katika kukimbia, na kuruka vikwazo mbalimbali na ambao waliibuka washindi ni  Vytautas Kirkliauskas na Neringa Kirkliauskiene raia wa Lithuania. 

 “ Nafikiri kwasababu tuna miezi mitatu pekee ya kuona mwanga tunahitaji kuwa na mashindano kama haya katika kipindi hiki na tunahitaji kumuonesha kila mmoja uwezo wetu", amesema  mmoja wa washiriki wa shindano hilo. 

Finland ni nchi ambayo ina baridi kali, jua huonekana kwa miezi mitatu pekee katika mwaka mzima na katika sehemu za kaskazini jua huzama kwa siku 73 mfululizo bila kuchomoza katika kipindi cha kiangazi na huchomoza kwa siku 51 bila kuzama katika kipindi cha masika. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad