Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na muandaaji wa muziki nchini Tanzania, Bob Junior amedai kuwa kwa mara ya kwanza kuonana na Diamond Platnumz ilikuwa ni mitaa ya Magomeni jijini Dar es salaam akiuza duka la nguo na yeye ndiye aliyeanza kumuomba amsaidie kurekodi kwenye studio zake za Sharobaro Records.
Bob Junior amesema kwa mara ya kwanza alipokutana naye alikuwa ana-rap lakini akamwambua aachane na huo muziki na ndio akarekodi wimbo wa nenda kamwambie.
“Wakati nakutana na Diamond ilikuwa mtaani tu maskani pale Magomeni alikuwa anauza duka la nguo, ikawa kila nikipita anasema Bob bwana nifanyie kazi, siunajua mimi nina roho tofauti ..! alikuwa ana-rap rap kwa akili yangu nikamwambia aachane na muziki huo yaani muziki wa ku-rap rap hapana tujaribu kuimba. Ndio akaja kamwambie ikawa kama ina U-RnB nikamwambia badilika kidogo imba Bongo Fleva zaidi, Then Alhamdulillah tukatoa wimbo ukawa mkubwa lakini kumbuka kwa wimbo huo kuwa mkubwa sijawahi kuchukua shilingi mia. Album yake yote iliyotoka nimelipwa nyimbo nyingine lakini Kamwambie sijataka nilipwe kwa sababu aliniomba na nikapenda anavyoimba so baraka zangu na baraka zake Mungu akaona kilio chetu, Diamond akawa mkubwa na mimi mkubwa na sharobaro ikawa kubwa.“amesema Bob Junior kwenye mahojiano yake na Wasafi TV.
Bob Junior ni moja ya Maproducer waliomsaidia Diamond Platnumz kabla ya kuwa na jina kubwa miaka ya nyuma na alishwahi kutengeneza Hit songs kadhaa ikiwemo Kamwambie na Kwetu Mbagala.
Sijalipwa Hata Shilingi Mia ya Wimbo wa ‘Kamwambie’ wa Daimond- Bob Junior
0
July 31, 2018
Tags